Skip to main content

ETHNOS_APP

Home • Search • Journals • List 0

Mchango wa Waandishi wa Kazi za Kubuni katika Uendelezaji wa Kiswahili

Bibliographic Data

ID21242373
AuthorsErnest Sangai Mohochi (0000-0003-1202-1901, Rongo University, corresponding author)
Year2019
Volume5
Issue3-4
Pages223-238
Publication date2019-10-02
Open AccessNo
TypeARTICLE
VenueEastern African Literary and Cultural Studies (JOURNAL)
Journal identifiersISSN: 2327-7408 • E-ISSN: 2327-7416
PublisherInforma UK Limited (PUBLISHER • GB)
DOI10.1080/23277408.2018.1529851
OpenAlexW2991438499
LanguageEN
References cited4

IKISIRIMakala hii ililenga kuchunguza mchango wa waandishi wa kazi za kubuni katika uendelezaji wa Kiswahili. Hili lilichochewa na ukweli kuwa waandishi ni miongoni mwa makundi muhimu katika ukuzaji wa lugha, mengine yakiwa: wanaisim, walimu, watafiti, wachapishaji, na wapenzi wa lugha. Hata hivyo, waandishi wa vitabu kuhusu maswala mbalimbali ya kinadharia, pamoja na uendelezaji wa lugha na fasihi yake ndio wametajwa zaidi. Mchango wa waandishi wa kazi za kubuni haujaangaziwa sana. Madhumuni mahsusi ya makala hii yalikuwa kuchanganua nafasi ambayo waandishi wa fasihi ya Kiswahili wameipa lugha hii katika kazi zao, pamoja na jinsi ambavyo nafasi hiyo inachangia katika ukuzaji wa lugha hiyo. Aidha, maelezo yametolewa kuhusu jinsi wamechangia kuwaathiri wasomaji wao kuhusu umuhimu wa Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya ushawishi wa kijamii inayoshikilia kuwa watu maarufu wana ushawishi mwingi unaowawezesha kuwaathiri wengine katika jamii. Waandishi wana sifa hizo na hivyo wanaweza kuathiri misimamo na mielekeo ya wasomaji wao kuhusu umuhimu wa lugha ya Kiswahili. Data ilikusanywa kwa kusoma kazi za kubuni za waandishi watatu wa fasihi ya Kiswahili walioteuliwa maksudi: Shaaban Robert, Wallah bin Wallah na Ken Walibora, pamoja na hojaji iliyotolewa kwa wanafunzi 40 na walimu 8 katika Chuo Kikuu cha Rongo. Vilevile, kazi za waandishi hao ziliteuliwa maksudi. Matokeo ya utafiti huu yameonyesha kwamba waandishi hawa wameipa lugha ya Kiswahili nafasi ya kipekee kama sehemu ya maudhui katika kazi zao, na wamewachora wahusika wapenzi wa Kiswahili wanaokitetea Kiswahili, ambao wanawaathiri wahusika wenzao. Isitoshe, waandishi hawa wameathiri msimamo wa wanafunzi na walimu wa Kiswahili kuhusu Kiswahili kutokana na nafasi wanayokipa katika kazi zao. Makala inahitimisha kuwa, kwa mujibu wa nadharia ya ushawishi wa kijamii, waandishi ni kundi muhimu katika jamii lenye ushawishi mkubwa na wanapoendelea kuithamini lugha ya Kiswahili, watawaathiri wengine wengi kuwa na msimamo kama huo

Theology · Education and Vocational Training · Educational Methods and Media Use · Philosophy

  • A Structural Theory of Social Influence

    Open Access•N E Friedkin•Structural Theory of Social…•1998

  • Social Influence and Sustainable Consumption

    Open Access•Elizabeth B Goldsmith•Social Influence and Sustainable…•2015

  • The New Public

    David Sciulli, Leon H Mayhew•Contemporary Sociology A Journal…•1999

Highly citedNo

Tools

Open DOISci-Hub
Ethnos_APP • Open Source Project • MIT License • Frontend v2.0.0 • Privacy and Cookies • API Documentation: api.ethnos.app/docs • API Source Code: GitHub • DOI: 10.5281/zenodo.17049435 • Frontend Source Code: GitHub • DOI: 10.5281/zenodo.17050053 • cruz.rio.br • Expectantes Misericordiae